Binadamu alivyoumbwa na Mungu anapaswa kujisitiri kwa kuvaa mavazi yatakayofunika mwili wake. Lakini mavazi haya hayapaswi kuvaliwa kwa muda wote (masaa 24 kwa siku), kutokana na sababu mbali, za kiafya au za kawaida kama ilivyo asili ya uumbaji. Nchi zenye ukanda wa hali joto ikiwemo Tanzania, kulala huku ukiwa umevaa nguo ni moja ya vitu hatari kiafya, kwani inaweza kusababisha madhara kiafya. Hapa nakupa sababu tano muhimu ambazo zitakazokufanya kuanzia leo usilale na nguo yoyote, na hii ni kwa faida yako mwenyewe. 1. Kulala vizuri Hapa inaeleweka wazi kisayansi kuwa ili ulale vizuri mwili wako unahitaji kutulia, upoe, na ndio maana tunaoga kabla ya kulala, ili kupunguza joto mwilini, ukiwa umevaa nguo mwili wako unabaki kuwa na joto, na kukufanya ukose usingizi na kukosa utulivu, lakini ukilala bila nguo, unaruhusu mwili wako kupata hewa ya kutosha na kusaidia kupoza joto la mwili, na kukupa usingizi mzuri zaidi. 2. Kuacha mwili upumue Kila sehemu ya mwili wetu umeundwa kwa seli...