Busu la mahaba liwe taratibu tena sio la mdomoni tu
RAHA ya mwanamke ni mume. Tena mume anayejua kumsambaza, kumgawa, kumsambaratisha na kumrusha roho yake kwa ufundi.
Lakini bahati mbaya sana sio wanaume wengi wanaojua wafanye nini kitandani kumridhisha mke, kama wao wenyewe wanavyoridhika.
Na matokeo yake wengi wao hawatendi yaliyo sahihi katika kumpa raha mwanamke. Kumtosheleza mwanamke kunahitaji utumie akili, mwili na ubunifu wa ziada ili uweze kuamsha hisia zake.
Wanaume wengi hufanya makosa kadha chumbani ambayo huwakosesha raha wake zao. Raha ambazo wangestahili kuzipata iwapo mwanaume angeepuka makosa hayo.
Nitachambua mambo kadha ambayo wanaume wengi wanapuuza, lakini ndio nguzo kuu ya kuamsha hisia za mwanamke.
Kuna yale mabusu, ambayo kaka zangu wengi huyapuuza wakidhani hayana maana yoyote. Ninaposema mabusu, simaanishi mabusu ya chap chap…la hasha. Busu la mahaba linatakiwa liwe taratibu na pia uelewe sehemu unazofaa kubusu. Naelewa kaka zangu wengi wanajua mdomoni pekee ndipo panapofaa kubusu, lakini sio mdomo na ulimi pekee ndivyo vinafaa kumumunywa, kuna maeneo mengine ya mwili.
Kwa mwanamke busu ni sehemu muhimu sana katika mapenzi kwani humaanisha una mapenzi ya dhati, unamjali na kumthamini na si mbinafsi katika masuala.
Lakini kaka zangu wengi mkishatumbukia kisimani, akili yote inahama na hata fikira za kumbusu tena mwenzake inapotea. Kubusu, kumwambia mwenzako maneno ya huba, kumwangalia machoni wakati wa burudani ni mambo ambayo huamsha hisia za ndani za mwanamke.
Rafiki zangu wengi hukosa raha ya mapenzi sababu waume zao wanashindwa kuvumilia kushiriki michezo ya mahaba kwa muda mrefu kabla ya kuingia shughulini.
Na mbaya zaidi ni mara baada ya kutumbukia kisimani, wengi wanashindwa kuhimili muda mrefu sababu ya ubinafsi na pupa nyingi. Iwapo ulikuwa huelewei umguse ama umbusu wapi mkeo, basi maeneo yafuatayo ni chachandu yanapoguswa na kupigwa mabusu kwa ufundi.
Shingo-Hii ni sehemu muhimu mno katika kuamsha hamasa za mapenzi ya mwanamke. Iwapo utaibusu kwa ufundi, uimumunye kiasi na kuipapasa kwa ustadi shingo ya mkeo, bila shaka utaona matokeo ya kuridhisha.
Nywele na masikio
Wanawake wengi hupenda mwanaume anayejishughulisha na nywele zake. Yaani anayejua kuzipapasa kimtindo, na kuzichezea. Kushikwa nywele kuna hisia za kipekee, ambazo mwanamke anazipata kwa kina zaidi akipapaswa na ampendaye. Nayo masikio ni sehemu yenye hisia kali. Sehemu hii inaleta raha zaidi ikipapaswa na ulimi. Yote haya yanahitajika kufanyika kwa ufundi, ubunifu na utaratibu.
Kuwa bubu wakati wa mahaba
Mapenzi ni starehe. Na kwenye starehe watu hawanyamazi, bali wanazungumza taratibu na kufurahia kile kinachowapatia starehe. Hivyo unaponyamaza na kuwa kama bubu kuanzia mwanzo wa burudani hadi mwisho, unapunguza ladha ya utamu wa huba. Tatizo hili liko zaidi kwa akina kaka, akishaingia shughulini, anaweka sura ya kazi, hazungumzi, hacheki, hanong'oni wala hatabasamu, anakunja sura kama vile anachimba mawe mgodini.
Hata hivyo ninaposema kuongea, simaanishi kubwabwaja maneno kama kinanda. Kwani kuna wale kaka zangu wasioisha kumuuliza mke, unakaribia kumaliza? Unajisikiaje? Umemaliza? Haya sio maswali ya kumwuliza mwenzako wakati mnaburudika.
Shughuli ikishamalizika, hapa huwa ni changamoto nyingine kwa wanaume wengi. Kwani kuna wale wanaogeuka upande mwingine na kuanza kung'orota, kuna wale wanaoinuka na kuondoka, labda kwenda kuangalia mechi ya mpira kwenye runinga.
Aidha kaka zangu wengi wanaogopa kuchemsha kitandani. Wengi wanapenda waonekane ni mafundi na hodari wa burudani. Na ndipo baadhi yenu mnakimbilia kuangalia picha za kurushana roho na halafu mnaenda kujaribu hizo staili kwa wake zenu.
Hizo staili zako ngumu ulizoangalia kwenye sinema, usimlazimishe mkeo ajipinde ili nawe uonekane kidume. Iwapo unataka staili mpya, zungumza na mkeo kwanza kabla ya kumshindilia na staili za sarakasi. Bila kujadiliana na kuamua kwa pamoja, hizo staili utazifurahia peke yako, kwani hakuna mwanamke anayefurahia kuingiliwa huku akiwa amekunjwa kama samaki.
Staili mpya inakuwa na raha iwapo nyote wawili mnakubaliana na mnaamua kuijaribu kwa pamoja. Lakini sio ukae sebuleni hadi usiku wa manane, uangalie sinema ya kurushana roho, ikuchemshe mwili, halafu unakimbilia chumbani na kuanza kumrusha mkeo kama mpira wa soka ukidhani atafurahia. Mwenye masikio na asikie. Habari ndio hiyo.

Comments
Post a Comment