MAMA VANESSA SEHEMU YA 11



Lucas na yeye hakutaka kufanya makosa alipeleka mdomo wake kwenye kinywa cha mama Vanessa. Alimbusu na kurudisha. Hakuwa na uhakika wa moja kwa moja kwani huyo mwanamke mke wa boss wake ameamua kujiachia na kuonesha yupo tayari kwa lolote. Kwa jinsi alivyokuwa mwanamke wa gharama isingekuwa rahisi hivyo kukubali kukutana na mtu wa chini kama Lucas.

“Nataka kuogelea”mama Vanessa aliropoka mara baaada ya kuangalia kwa muda mrefu maji ya ziwa na jinsi ambavyo watu walikuwa wakiogelea pembezoni mwa kisiwa hicho. Lucas alitafakari kidogo na kumwambia hasiwe na hofu ngoja akachukue boti ya mwendo kasi.

“Wewe mimi boti naogopa”

“Usiogope upo na mimi” Lucas alijibu huku akiondoka na kuelekea sehemu ambapo viboti hivyo vilikuwepo. Hakuwa na wasiwasi maana haikuwa mara yake ya kwanza kula bata eneo hilo.Hili kumuondoa hofu mama Vanessa, Lucas alilipanda kishakuingia ziwani. Aliweza kuliendesha kwa madaha huku akikata mwaimbi ya ziwa mpaka sehemu za mbali kidogo. Alifanya mbwembwe zote kuonesha yeye ni mwanaume ambaye haogopi maji. Mama Vanesaa alitumbua macho na kuona kweli mwanaume huyo ni mtaalamu wa kuchezea maji. Baadaye Lucas alikuja na kumpa mkono ili apande.Mama Vanesa alisita kidogo lakini alipiga moyo konde na kuingia kwenye boti. Walianza kuzunguka ziwa huku wakikata mawimbi.Mama Vanesaa alimshika vilivyo kwenye kiuno ili hasije akaanguka.Walifurahia maji na kwa kweli zile pombe ziliyeyuka. Mama Vanesaa alijihsi yupo dunia ingine kabisa maaana tangu aolewe amekuwa mtu wa kubanwa na hakuwahi kufurahia maisha kwa namna hiyo.

Walirudi sehemu waliyokuwa wamekaa. Wote walikuwa na nguo za mama Vanesa zilikuwa zimelowana. Ujue Lucas alipinguza nguo na kubaki na bukta lakini mama Vanesa yeye hakupnguza kitu. Lucas alikuwa ameliona hilo hivyo alimuuliza kama amekuja na nguo zingine.

“Vipi mama Vanessa umekuja na nguo zingine ili ubadilishe hizo maana naona umelowana.”

“Mwanamke lazima ubebe nguo zingine lakini shida nitabadilishia wapi.”

“Twende kule hotelini kuna chumba nilikuwa nimechukua.”

“Mmmh ulichukua chumba kwani umepanga kulala hapa?. Mimi mwenzio baba Vanesaa ataniua natakiwa nirudi leo nyumbani”

“Hapana mimi sitolala hapa nitaenda kulala kwa rafiki yangu, hicho nimekuchukulia wewe ili ukapumzike kama muda utakuwa umeenda sana. Sasa hivi tayari ni saa kumi na mbili sasa huoni kuwa utachelewa.

“Ni kweli lakini umewezaje kulipia chumba cha ghali hili hali huna kazi maisha yako yao hatariini huna pesa?”

Lilikuwa swali kumbwa ambalo hakulitarajia. Hapo alikosa jibu akanyamaza kimya huku simu yake ikiita na kuangalia alikuwa ni Kimaro akipiga. Alishindwa kuipokea na badala yake alitoa funguo na kumkabidhi mama Vanesa.

“Huko mikono salama nenda chumba namba tano badili nguo then urudi tupange mikakati na muda ukiruhusu basi utarudi”. Lucas safari hii alionekana kubadilika kidogo. Mama Vanesa hakutaka kupingana naye alijinyanyua hapo na kuanza kuelekea huko alipoelekezwa. Hapakuwa mbali sana hivyo alipiga hatua zake za madaha na kumuacha Lucas akimsindikiza kwa macho. Mmacho ya Lucas yaliendelea kukiri kuwa mwanamke huyo ni miongoni mwa wanawake wazuri na warembo huku duniani. Baada ya mama Vanesa kuondoka ilikuwa ni nafasi nzuri kwake kunynyua simu yake na kumpigia Kimaro. Kimaro alimweleza kuwa yupo eneo hilo na yupo na kimwana ..

“Upon a Julieth?Lucas aliuliza kwa kuhamaki.

“ Aaaaaah kwani umeambiwa kimwana ni Julieth tu.”

“Sijamaanisha hivyo ila ukimleta huyo atatuona sisi wote ni Malaya tu na imani yake juu yako itapungua.Lucasa alijaribu kueleza wasiwasi wake.

“ Ebu wacha maneno mengi nishafika hapa naingia umekaa kwa wapi?.

“Huku karibu na ziwa kabisa”

“Sawa dakika sufuri”.

Baaada ya nusu dakikaa Kimaro aliingia eneo hilo huku akiongozana na msichana mwingine ambaye yeye alimwita kimwana. Alikuwa ni mwanamke mrembo kwa maana nachelea kusema ni mzuri sana. Maana uzuri ni tofauti na urembo. Uzuri ni kitu ulichozaliwa nacho ni kutokana na uuumbaji wa Mungu. Urembo ni jinsi ulivyojitengneza kuanzia mwonekano, mavazi na mapozi. Alikuwa ni mwanamke mrembo na alivutia machoni pa Lucas.

“Yani huyu kwa kubadili wanawake kama nguo.. Sasa amempata wapi na huyu?” Lucas aliwaza mara baada ya kuwaona wakiingia kupitia boti ambalo lilikuwa linawavusha watu kutoka nchi kavu na kuwapeleka kwenye kisiwa hicho. Kilikuwa ni kisiwa ambacho hakikuwa mbali sana na nchi kavu na hakikuwa kikumbwa zaidi kilikuwa na hote hiyo na sehemu zilizojengwa kwa ajili ya utalii.. Aliwapungia mkono na wao walimwona. Hao kwa mwendo wa madaha kama mtu na mpenzi wake walijisogeza eneo hilo. Walifika na kuvuta viti kukaa. Walikuwa wenye furaha na waliochangamka sana. Kwa kuwa viti vilikuwa ni vichacahe n kilea alichokuwa amekalia mama Vanesa kilishatumika ilimlazimu kumwita muhudu ili awasikilize wageni na aongeze kiti kimoja.

Muhudumu aliwasikiliza na kwenda kuchukua vinywaji. Mara Mama Vanesa naye alikuwa akija kutoka kwenye hotel. Alichukua muda mrefu lakini haikuwa tatizo kwa Lucas maana anajua kabisa wasichana linapokuja swala la kubadili nguo lazima waanze kujiremba upya. Ni kweli maana mama Vanesa alikuwa amebadilika kabisa na kuzidi kuonekana kuwa alikuwa ni msichana mdogo. Alivaa kimini kilichofanya kuacha mapaja yake nje. Alionekana ni binti mdogo pengine waweza kusema ni msichana amabye hajaolewa. Lucas hakujua kwa nini amevaa hivyo lakini huenda labda aliamua kujiachia mara baada ya kuhisi kuwa watakuwa wawili tu. Hakujua kama kuna wageni wanaweza kuja. Hata hivyo hakuonesha kushtushwa sana alivuta kiti na kukaa. Kimaro aliyatumbua macho na hakuamini kama huyo ndo mke wa boss ambaye alikuwa akizungumziwa..
ITAENDELEA. ....



Comments

Popular posts from this blog

Jinsi Ya Kumtambua Mwanamke Mwenye Nyege

JINSI YA KUCHEZEA MATAKO YA MWANAMKE NA KUMPA RAHA YA AJABU KWA KUYABINYA KATIKA MIELEKEO MAALAM SOMA HAPA

Kanga Moja....Ndembe Ndembe. Sehemu ya Kwanza