MAMA VANESSA SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA
“No no I say no I cant tolerant any more(hapana, hapana nasema hapana siwezi vumilia tena)..” Lucas alinyanyuka kwa nguvu na kuanza kuelekea kule mbele ambapo boss na mkewe walikuwa wanacheza
ENDELEA
Kimaro ambaye na yeye alionekana kuwa tayari ameshalewa alinyanyuka kwa nguvu na kumshika Lucas. Alitumia nguvu zake zilizochagizwa na pombe kumzuia na kumsogeza kwa pembenni.
“Ndugu yangu nakuomba unisikilize kwa umakini sana kwa sababu ulimwengu huu sio wa kutumia nguvu bali akili. Huyo ni mke wako sawa najua anauma kuliko kitu kingine chochote ila sasa yupo na boss wako na wewe umesimamishwa kazi tu. Kitu cha kujua ni kwamba hujafukuzwa kazi bali umesimamishwa kazi hivyo lazima uwe mjanja ili kurudishwa kazini ikibidi huyo boss yeye ndo afukuze..
“Nifanyaje sasa”, Lucas alihoji kwa kuvuta pumzi..Hasira zilimshuka kidogo.
“Unatakiwa kutumia akili . Kwa kuwa Boss wako yupo na mkeo hapa tupate ushahidi wa picha. Tukishapata ushahidi huo ni rahisi sana kuieleza jamiii kuwa boss amekunyanyasa na anatoka na mkewe na pia anatumia fursa hiyo kukufukuza kazi.”.
“Wazo zuri sana sasa utawezaje kuwapiga picha bila wao kujijua na bila kuleta madhara maana yule boss ni mkorofi sana”
“Hilo niachie mimi wewe rudi kakae.Vaa roho ya ushujaa na uwe na amani kwa sababu huu mchezo sisi ndo tutashinda.
Lucas Manyama alionesha kuelewa na alirudi kukaa kwenye kiti na alishangaa kukuta kuna msichana mwingine amekaa kwenye kiti chake. Macho hayana pazia kwa sababu msichana huyo alikuwa akifanana kabisa na msichana wa mwanzo. Kwa haraka haraka aliwaza na kugundua kuwa anaweza kuwa ni pacha wake. Manyama alivuta kiti na kukaa.Alielekeza macho yake mbele na kuangalia kwa makini kama kweli rafiki yake Kimaro anaweza kufanikisha kuwapiga picha. Hakumwona hata huyo Kimaro jambo ambalo lilizidi kumchanganya.
“Shemeji usiwe na wasiwasi wala usiwaze sana wanawake bado hawajaisha huku duniani na kama kweli yule ndo mkeo na anayafanya yale huku wewe ukiangaika kumtafuta ili kujua alipo basi huna chako.”
Yalikuwa ni maneno ambayo yalizidi kumuuma Lucas na kutamani kama angefanya kitu. Bila kutarajia alinyanyuka na kusimama. Aliwaza kutoweka eneo hilo na kwenda sehemu nyingine kabisa mbali na upeo wa vitu vya kuumiza vilivyokuwa vikiendelea. Kimaro alimshika begani na kumwambia arudi kukaa.
“Vipi umekamilisha huo mpango?”.
“Nimekamilisha kwa kiwango kikumbwa”.Kimaro alijibu huku akimpa simu yake ili aweze kuangalia. Aliziona picha na jinsi mkewe alivyokuwa amekumbatiwa na boss wake. Alishindwa kujizuia machozi yalimtoka.
“Jamani Lucas usiwe na roho ndogo hivyo wewe ni mwanaume usilie jipe moyo”alisema Yule msichana aliyekuja mara ya pili.Msichana huyo aliongea kwa upole huku akitoa kitambaa chake na kumpa afute machozi. Lucas alisista kukichukua lakini mwanamke huyo kwa ujasiri alijisogeza zaidi na kumfuta machozi. Ilikuwa ni faraja kwa Lucas kwani alichukua glass akaminiia kinywaji chake na kunywa. Alikunywa kwa nguvu kisha kushusha chini. Aligonga meza kwa nguvu kuwa aongezewe kinywaji. Muhudumu alikuja na kumuongezea. Sasa ilikuwa ni kunywa kwa nguvu ili kutafuta stimu za kupunguza mawazo. Kila mtu alikunywa kadri alivyoweza na nikama boss na mke wa Lucas walishtuka na kutoweka ghafla eneo hilo. Wao wakabaki wanaendelea kula raha na kujaribu usahau shida ambazo walikuwa nazo.
“Sasa ni saa ya utambulisho, kila mtu akae kimya” aliropoka Kimaro.
Watu wote walicheka maana kumbe wengine hapo mezani walikuwa hata hawafahamiani. Kimaro akanza kujitambulisha yeye.
“Mimi naitwa Godfrey Kimaro kijana mdogo mwenye mafanikio hapa mjini”.Wote kwa pamoja walitabasamau.
“Mimi naitwa Lucas Manyama mwanaume ambaye namiliki mke mzuri mjini lakni Boss akanipokonya”..Hapo kila mtu akaangua kicheko huku Lucas akitingisha kichwa kuonesha masikitiko yake juu ya jambo hilo.
“Mimi naitwa Julieth mpenzi wa kijana mwenye mafaniko hapa mjini”
“Mimi naita Juliana pacha wa Julieth”.
“Safi sana sasa timu imekamilika na hatuwezi kukubali mziki uishie chini. Kila mtu amshike mtu wake tunaenda mbele kucheza.” Kimaro aliongea huku akimnyanyua Julieth. Pombe ilikuwa imekolea na hao taratibu walisogea mbele kwenda kucheza mziki na kuwaacha Lucas na Juliana wakiwa wanaangaliana.Juliana hakuwa na aibu maana na yeye pombe ilikuwa imekolea. Alisimama akajitingisha tingisha kidogo kwa madaha nakuonesha ni jinsi gani alivyoumbwa akaumbika. Macho kodoo macho ya Lucas yalimkodolea huku akimkagua kuanzia kifuani kushuka chini. Juliana akanyanyua mkono mmoja kisha akampatia ishara kuwa wanyanyuke. Lucas alikuwa ni mtu mwenye aibu sana hivyo alikuwa akijifikiria kwenda mbele kucheza muziki. Lakini mikono laini ya Julaina ilitosha kumsisimua na kumuinua kutoka pale kwenye kiti.
Hao walisogea mbele na kuanza kucheza. Mbele kulikuwa na watu wengi hivyo ilikuwa ni swala la kubambia kwa kwenda mbele. Sasa ilikuwa ni fursa ya Lucas kuona ulimbwende wa binti huyo. Kwa kweli alichanganyikiwa na alitamani hata kumtongoza usiku huo huo. Alijizuia lakini kitendoa cha Juliana kuzungusha nyonga na kumtingishia makalio kilimfanya kumtamani mlimbwende huyo. Juliana naye alimwonea sana huruma na aliamua kumfanyia vitu ambavyo vingempa faraja usiku huo. Alikuwa akicheza na binti huyo huku mawazo yake yakiwa kwa mtu aliyejitambulisha kuwa anaitwa Mama Vanesaa. Aliifikiria ile sauti ambayo ilionekana ya binti mdogo kabisa na jinsi mwanamke huyo alivyoamua kujitambulisha kwa jina mama Vanesa. Baadaye walirudi kukaa na sasa walikuwa wameagiza nyama choma. Walikula na wakati wakiendelea kula simu ya Lucas iliita na kuangalia alikuwa ni mama Vanesa. Alikata na kumuomba amtumie sms kwa kuwa yupo kwenye kelele.
“Nimepata dharura ambayo itanifanya kesho kutwa nisafiri hivyo nilikuwa naomba kama hutojali tukutane kesho nikueleze matataizo yangu kisha tupange mikakati ya kusaidiana kwa sababu matatizo yako tayari nayajua.” Meseji kutoka kwa mama Vanesa ilisomeka hivyo.
“Kula brother nataka nikupe huyu mtoto Juliana ukalale naye upunguze hata mawazo.”Iliingia meseji ingine kutoka kwa Kimaro.
Alitabasamau kimoyomoyo na kujisemea kama litataokea hilo basi itakuwa bahati ya mkenge. “Mtoto mzuri hivyo nitamla mpaka aimbe zeze”aliendelea kuwaza huku akiweka finyango ya nyama mdomoni.Mara Juliana na yeye alichukua nyama na kumlisha jambo lililozidi kumsisimua na kujikuta akitamani hata kumrukia muda huo. Viungo vingine vya mwili navyo vilishasimama kwa hisia za mahaba…********ITAENDELEA*********
UMEONA? UMEONA LAKINI BRAZA SIKUSEMA MKUKI MTAM KWA NGURUWE... UNAMIND MKEO ALAFU WEWE UNATAKA MPAKA KURUKIA WATU HAHAHAHA.... ATAIMBA ZEZE AU SIO BRAZA LUKA??? TUNASUBIRIIIII ILO ZEZE...

Comments
Post a Comment