MAMA VANESSA SEHEMU YA TISA

Yaani alijikuta akianza kutetemeka bila yeye kupenda. Hukujua kwa nini mkewe alikuwa akimpigia wakati huo. Alishindwa kabisa kuamini kama mkewe ambaye alikuwa hapatikani takribani wiki mbili sasa ndo huyo alikuwa akimtafuta. Alisita kuipokea na aliiacha maana tayari hasira zilikuwa zimempanda kupita kiasi.Baada ya yeye kukataa kupokea simu kwa hiyari yake kuna sms iliingia.
“Kwa mjinga huenda kicheko kwa mwelevu huenda kilio.Nashukuru kwa kutopokea simu yangu. Ila tambua mimi ni mke wako wa ndoa na hakuna cha kututenganisha.”
Lucas alirudia kuisoma ile SMS na kujikuta akizidi kuchanganyikiwa maana maisha yalikuwa yakimchanganya kwa kiasi kikumbwa.Alitamani hata kulia lakini alilia machozi yaliyoishia ndani ya moyo wake. Kijasho chembamba kilimtoka na kujikuta akiwasha feni ili hewa iiingie. Bado hakupata hafueni na akaamua kutoka nje kabisa. Alikuwa kifua wazi huku akitamani hata kunywa pombe. Alikaa hapo kwenye kibaraza cha nyumba. Mawazo ya uchngu yalizidi kuunyanyasa ubongo wake. Moyo wake ulizidi kunyong’onyea kwa hasira ya mambo ambayo yalikuwa yakiendelea. Alitamani ardhi ifunguke na yeye aingie ndani. Maisha kwake yalikuwa ni mtihani mkumbwa sana ambao kwa kweli uliitaji nguvu za ziada kukabialiana nao. Nyumba aliyokuwa akiishi ni nyumba ambayo ilikuwa ikiongozana na Lodge. Kwa hiyo wakati akiwaza na kuwazua macho yake aliyaelekeza moja kwa moja kwenye lodge hiyo. Aliona gari likiingia eneo hilo na ni kama vile alikuwa akilitambua gari hilo ni la boss wake. Alishangaa kwa sababu walivyoachana na mama Vannesa boss huyo alieleza kuwa amefika nyumbani kutoka Mwanza kwenye semina.
Ilimlazimu kusimama maana alihisi kama amefananisha hilo gari. Kwa kuwa yeye alikuwa gizani hakuwa na hofu sana maana mtu alaiye kwenye mwanaga ilikuwa ni ngumu sana kumwona. Alishangaa kuona boss wake huyo akishuka na mwanamke mwingine ambaye na yeye hakuhitaji mwanga wa mchana kujua kama alikuwa ni mrembo. Alitamani hata kuwapiga picha lakini wahusika hao waliingia kwa haraka sana. Wazo lilomjia ni kumpigia simu mama Vanesa na kumuuliza kama mumewe alikuwepo nyumbani au la. Aliingia ndani na kuchukua simu yake ambayo alikuwa ameiweka chaji. Alipiga namba za mama Vannesa lakini kwa bahati mbaya simu hiyo haikupokelewa. Haikuwa usiku sana lakini alishindwa kupiga tena kwa imani kuwa huenda ni usiku na yupo na mumewe. Aliamua kuamini kuwa alichokiona haikikuwa sahihi na zaidi ilikuwa ni hisia zake tu. Alitamani kwenda mpaka kwenye ile lodge lakini alikuwa na hofu huenda akaanza kuulizwa maswali mengi na mlinzi.
Kwa kuwa ndani kulikuwa na joto alirudi zake nje na kuendelea kutafakari mustakabali wa maisha yake. Roho iliendelea kupwitapwita kwa kuuma na kutamani kama angekuwa na nguvu ya kupambana na huyo boss. Pamoja kuwa wana pesa sitokubali kwa njia yoyote ile nifukuzwe kazi. “Afanye yote lakini sitokubali kwa maana kama anatembea na mke wangu na mimi nitatembea na mke wake. Sio mke wake tu hata mtoto wake. Nipo tayari hata kufa lakini sio kudhalilishwa kwa kiasi hiki kikumbwa. Mke anauma sana na sijui kwa nini nimeweza kuvumilia kwa kipindi chote hicho. Nitaenda hata kwa mganga kumloga. Maisha ndo haya haya kwa kweli sipo tayari kwa namna yoyote ile kudhalilika kisa madaraka au pesa.” Lucas aliyawaza hayo kisha akakunja uso wake kwa nguvu. Alikunja pia ngumi yake kwa nguvu akaizungusha kwenye uso na kuing’ata.
Usiku uliendelea kuwa mgumu sana kwa bwana Lucas Manyama. Kwa sasa alikuwa akisubiri kwa hamu kumbwa hiyo kamati ya nidhamau na maadili ya kazini kwao. Maisha yaliendelea huku akimwomba mwenye nyumba amvumilie kwa mwezi huo kwani mambo hayakai sawa kwa upande wake. Mwenye nyumba alimweleza bayana kuwa hatoweza kumvumilia zaidi ya mwezi hivyo kama hawezi kulipa kodi basi atafute kitu kingine cha kufanya. Zilikuwa ni kauli za kuumiza lakini alijikaza kama mwanamume na kuamini hizo ni changamoo za maisha na huwa zinakuja kwa nayakati na kuondoka na pengine kusaulika. Siku zilizidi kuyoyoma na hatimaye siku ya kusikiliza shitaka lake ilifika akaitwa. Alifika na kusikilizwa na inaonekana boss alijipanga sana maana utetezi wake haukufua dafu mbele ya kamati hiyo. Maamuzi yakatoka kuwa ataendelea kusimamishwa kazi mpaka hapo atakapo lipa deni la million 5 ambalo yeye amesababishia kampuni hiyo. Alitamani kutoa ya moyoni mwake kuwa boss alikuwa na uhusiano na mfanyakazi mpya ambaye na yeye alianza kuwa uhusiano naye lakini roho moja ilimwambia inampasa kukaa kimya maana anaweza kuharibu kabisa.
Lucas alijijengea katika maisha kuwa kamwe hasifanye maamuzi akiwa na hasira au akiwa hana mtu wa kumsapoti. Alitamani sana kuelezaa kamati hiyo ya maadili ya mabaya yote ambayo amefanyiwa na boss. Alitamani kuwaambia kuwa mfanyakazi mpya aliyekuja ndio chanzo cha ugomvi. Alitamani kueleza kuwa boss amemwaribia maisha kwa kumchukua boss wake. Hasira zilimpanda sana na bila kutarajia aliamua kuondoka hili hali kikao kilikuwa bado kinaendelea.
“Ndugu zangu kwa sasa nina hasira sana ambazo zimechanganyika na uchungu wa kile ambacho kilikuwa kikitokea.. Nina mengi sana ya kuwaeleza kwa kuwa mmeshindwa kunisikiliza naomba nitawakilisha ushahidi wangu wa picha na vitu vingine kuonesha ni jinsi gani nimeonewa sana na nimedhulumiwa haki zangu za msingi. Nimekuwa nikipitia kwenye kipidi kigumu sana na naamini kama kamati ya ndani ya maadili ikishindwa kunitetea basi nitaenda idara ya kazi” Lucas aliyasema hayo kisha akapiga ngumi kweye meza na kuanza kuondoka zake. Hakika alionesha kufadhaishwa sana na kilichojadiliwa hapo na kumfanya aonekane ana mengi sana moyoni lakini hana imani na sehemu hiyo. Alishindwa kuyawasilisha kwa kukosa imani na kamati ya maadili. Kamati ambayo ilikuwa imetengenezwa na boss kamati ambayo ipo radhi kupindisha ukweli kamati ambayo ipo tayari kwa gharama yoyote kulinda maslai ya kampuni.
Lucas Manyama aliondoka na kurudi nyumbani. Alikuwa ni mtu mwenye hasira sana na alichokifanya ni kununua pombe kali na kunywa. Alikunywa viroba japo huwa hapendi kabisa kunywa. Aliingia ndani na kulala. Alifanikiwa kupata usingizi akalala na alikuja kushtushwa na njaa ambayo ilikuwa ikimkabili. Alijinynyua na kwenda kutafauta kitu cha kula. Alikula na baaada ya hapo alaipata fusa ya kutafakari yote yaliyotokea kwenye kamati ya maadili. Limshukuru Mungu hakuweza kutoa ya moyoni maana anageweza kuchafua hali ya hewa na kufanya hata watu wapigane.Aliwaaambia yaliyojiri na wengi walimshauri kuwa awe mvumilivu kwa kipindi hiki na pia awaambie hiyo kamati yao impe kwa maandishi kila walichokijadili na maamuzi yake ili wasije mgeuka kipindi atakapoeenda idara ya kazi. Alikubali kufuata ushauri huo na akaseam kesho ataenda kazini. Baada ya kuongea na washauri wake kuna namba ngeni iliyokuwa ikimpigia , aliamua kuipokea.
“Helow mpenzi nimekumiss sana na siamini kama kweli umefika Musoma na hujataka kunitafuta.” Lucas alitega sikio kwa umakini sana na kufanikiwa kugundua kuwa alikuwa ni Juliana.
“Samahani sana mwenzio sipo sawa kwa kweli yaani maisha yananichanganya. Sio mimi ni maisha tu ndo yamenifikisha hapa.” Lucas aliongea kwa sauti ya upole.

****ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi Ya Kumtambua Mwanamke Mwenye Nyege

JINSI YA KUCHEZEA MATAKO YA MWANAMKE NA KUMPA RAHA YA AJABU KWA KUYABINYA KATIKA MIELEKEO MAALAM SOMA HAPA

Kanga Moja....Ndembe Ndembe. Sehemu ya Kwanza