Wanawake Huvutiwa na Mwanaume Mwenye Sifa Hizi
Wanaume wengi humuona mwanamke kuwa ni fumbo gumu ambalo ni vigumu kuamiliana nalo, lakini ukweli wa mambo ni kinyume na mtazamo huo. Mwanamke hutafuta sifa maalumu kwa mwanaume zinazoendana na shakhsia yake. Kiujumla kuna aina kadhaa za wanaume ambao huwavutia wanawake, kama zinavyoletwa kwako:
- Mwanaume Romantic: Muhibu wa aina hii anayezijali sana hisia za mwanamke humvutia sana mwanamke. Anapomletea zawadi, akamfanya kuwa mwenye furaha muda wote, huwa kivutio maridhawa cha moyo wa mwanamke kwa sababu humpenda mtu anayemthamini na kumpa umuhimu muda wote.
- Mwenye Anajiamini: Mwanaume anayemfanya mwanamke ahisi amani, akajiamini na kuiamini shakhsia yake, huyo huweza kumfanya mwanamke avutiwe naye, hasa kutokana na ukweli kwamba mwanaume wa aina hiyo ni mchache wa wivu kuliko wanaume wengine.
- Mbunifu: Mwanaume anayeweza kubuni njia za kumshangaza na kumstaajabisha mwanamke hupendwa sana, kwa sababu mwanamke hupenda ahisi kuwa yeye ni maridhawa na wa kipekee.
- Mcheshi: Mwanamke humpenda mwanaume anayeweza kumchekesha na kupandikiza tabasamu usoni mwake, hasa katika kipindi ambacho anakuwa mwenye huzuni. Watafiti wameeleza kuwa mwanamke anaweza akafumbia macho aibu nyingi za mwanaume iwapo ana sifa hii ya ucheshi na mwenye uwezo wa kumfurahisha.
- Mwenye Anamdekeza: Mwanamke humpenda mwanaume anayemdekeza, akamfungulia mlango wa gari au nyumba, akamsogezea kiti, akaamiliana naye kwa ulaini na kuheshimu hisia zake. Huyo atapata nafasi kubwa ya kupendwa kuliko mwanaume mbabe, mkali na asiyemdekeza.
Mwanaume ukijitahidi yafuata haya hakika utakua kama ua ridi ambalo kila Mwanamke utae kutana nae hatatamani kukuacha uondoke bila kukupa fursa ya kumtibu moyo wake.
Comments
Post a Comment